Campbell aamrishwa kuwepo kesi ya Taylor

Naomi Campbell
Image caption Naomi Campbell

Mahakama ya kivita ya Sierra Leone imemuamrisha mwanamitindo mashuhuri wa kimataifa Naomi Campbell akatoe ushahidi katika kesi dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia , Charles Taylor.

Inadaiwa mwanadada huyo alipokea pandikizi la almasi kutoka kwa Bw Taylor kama zawadi kwake miaka 13 iliyopita.

Waendesha mashataka wanadai Campbell alitunukiwa "almasi ya damu" mnamo mwaka 1997 nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela.

Bwana Taylor anashutumiwa kutumia almasi kama hizo kuchochea vita nchini Sierra Leone.

Bi Campbell ambae ni raia wa Uingereza alikwishawahi kukataa kutoa ushahidi wowote kuhusu kesi hio lakini sasa ameamrishwa afike katika mahakama hiyo mjini the Hague Julai 29.

Mnamo mwezi wa Aprili aliondoka kwa hasira kutoka kituo kimoja cha televisheni wakati alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Charles Taylor -- akiangusha kamera ya kituo hicho.