Mawaziri kujadili mishahara ya wabunge

Rais Mwai Kibaki
Image caption Rais Mwai Kibaki

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki baadaye leo asubuhi anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kujadili pendekezo la wabunge wa nchi hiyo la kujiongezea mishahara na kuwa miongoni mwa wabunge wanaolipwaa kiasi kikubwa zaidi cha mshahara duniani.

Ikiwa pendekezo hilo litaidhinishwa na rais Kibaki kuwa sheria, wabunge hao watapokea dola lefu mia moja hamsini kila mwaka kama mishahara.

Lakini viongozi wakuu wa serikali akiwemo Waziri Mkuu Raila Odinga wamepinga pendekezo hilo. Bw. Odinga amesema pendekezo hilo la wabunge, limetolewa wakati mbaya ambao wakenya wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Image caption Mkenya akipelekwa hopsitalini

Vyama vya wafanya kazi pia vimetishia kuongoza mgomo ikiwa rais Kibaki ataidhinisha pendekezo hilo kuwa sheria.

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo, Francis Atwoli, amesema ni aibu kwa wabunge hao kupitisha mswada wa kuongeza mishahara yao, ili hali walipinga mswada uliowashinikiza wabunge hao kulipa ushuru.