Viongozi wa Upinzani kustakiwa Rwanda

Benard Ntaganda
Image caption Benard Ntaganda

Viongozi 9 wa upinzani nchini Rwanda, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kuandaa maandamano bila kibali kutoka kwa serikali.

Miongoni mwao ni Bernard Ntaganda, mwanzilishi wa chama cha Social Party-Imberakuri ambaye pia ni mgombea urais wa chama chake cha upinzani .

Maandamano hayo katika mji mkuu wa Kigali, yalinuiwa kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuruhusu vyama kadhaa vya upinzani kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Upinzani umeilaumu serikali ya Rais Paul Kagame, kwa kuizuia kuendesha shughuli zake bila vikwazo.