Maaskofu wanawake waruhusiwa - Uingereza

Image caption Aksofu mwanamke wa kanisa Anglikana

Kanisa la Kianglikana nchini Uingereza limechukua hatua kuwaruhusu wanawake kuhudumu kama maaskofu licha ya onyo kutoka kwa viongozi wao wenye itikadi kali kuwa watajiondoa kutoka kwa kanisa hilo.

Viongozi hao wamesema kuwa hatua hiyo inaenda kinyume na mafundisho ya bibilia yanayokataza wanawake kuwa maaskofu.

Hata hivyo baraza kuu la kanisa hilo, Synod, limekanusha hilo na kupania kuwapa wanawake haki sawa na wanaume katika uongozi wa kanisa.

Kiongozi wa kanisa hilo, askofu mkuu wa Canterbury Rowan Williams amekiri kuwa kuna changa moto kuu la kushikilia kanisa pamoja kwani migawanyiko imekithiri katika kanisa hilo.

Image caption Askofu Williams

Suala hilo limezua utata miongoni mwa jamii nzima ya kianglikana kote duniani.