ICC - Hati ya pili ya kukamatwa Bashir

Image caption Rais Omar Al Bashir wa Sudan

Mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC imetoa hati ya pili ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir. Hati hiyo imetolewa kwa kosa la pili la mauaji ya kimbari.

Kiongozi wa mashtaka mwandamizi wa mahakama hiyo Louise Moreno Ocampo amemlaumu Bashir kwa kuhusika katika kuchochea mauaji ya makabila matatu mjini Darfur kusini mwa Sudan.

Hati ya awali kutoka kwa mahakama hiyo iliyotolewa mwezi Machi mwaka uliopita ilimwekea Bashiri mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Hata hivyo mshirika mkuu wa Rais Bashir Rabie Abdelatif ametaja shtaka hilo kama upuzi mtupu.

Marekani ilitoa wito kwa rais Bashir ajiwasilishe kwa mahakama hiyo ya ICC kujibu mashtaka yanayomkabili.

Image caption Rais wa Sudan Omar Al bashir

Zaidi ya watu 3,000 wanadaiwa kuuawa katika eneo la Dar Fur tangu mapigano kuzuka mwaka wa 2003.