Hatukumteka mwanasayansi wenu - Clinton

Image caption Shahram Amiri anayedai kutekwa na Marekani

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa mwanasayansi wa Nuclear wa Iran anayedaiwa kutekwa na maafisa wa Marekani CIA alijipeleka mwenyewe nchini humo na siku zote amekuwa huru kurejea nyumbani.

Badala yake alishutumu kuzuiliwa kwa wamarekani watatu mjini Tehran.

Mwanasayansi huyo Shahram Amiri aliwasili katika idara inayoshughulikia masuala ya Iran katika ubalozi wa Pakistan mjini Washington baada ya kutoweka kwa zaidi ya mwaka mmoja kutoka nchini Saudi Arabia.

Image caption Waziri Hillary Clinton

Lakini katika mahojiano na wanahabari, bwana Amiri alisisitiza kuwa alitekwa nyara na kuwa anashuku kuhusika kwa Israel.