Makabiliano kwa siku ya tatu - Ireland

Image caption Machafuko nchini Ireland

Mapigano yameendelea kwa siku ya tatu nchini Ireland ya kaskazini ambapo waandamanaji wamekabiliana na polisi wa kuzuia ghasia licha ya wito wa amani kutoka kwa wanasiasa na viongozi wa serikali.

Duru zimearifu kuwa risasi zilifyatuliwa dhidi ya polisi hao ambao walirushiwa pia mabomu ya petroli katika mji huo wa kaskazini mwa Belfast, ulio na waumini wengi wa dhehebu la Katoliki.

Maandamano hayo yanatokea wakati wa sherehe za waumini wa dhehebu la Protestant wanaounga mkono utawala wa Uingereza kaskazini mwa Ireland.

Waandamanaji hao wanapitia katika maeneo yaliyo na wafuasi wengi wa dhehebu la katoliki wanaopinga utawala wa Uingereza huko.