Al Shabaab kamwe hawana utu - Obama

Image caption Rais wa Marekani, Barack Obama.

Rais Barack Obama amesema kuwa kundi la wapiganaji wa Al Shabaab linalojigamba kuhusika na mashambulio yaa mabomu nchini Uganda halithamini maisha ya waafrika wenzao.

Obama alisema kuwa inahuzunisha kuwa shambulio hilo lilitokea wakati watu wanasherehekea tukio muhimu kama Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini.

Awali balozi wa Marekani nchini Uganda, alisema kuwa kuna haja ya kuongeza usaidizi wa kijeshi wa Marekani nchini Uganda kufuatia shambulio la kigaidi lililofanyika nchini humo.

Balozi Jerry Lanier amesema kuwa shambulio hilo ni ishara kuwa kundi la wapiganaji wa Al Shabaab linalenga hata raia nje ya Somalia.