Mapigano Congo: 40,000 watoroka makwao

Image caption Mapigano mapya nchini Congo

Shirika la misaada la Oxfam limesema kuwa zaidi ya watu elfu arobaini wametoroka makwao kaskazini mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuatia mapigano kati ya jeshi la nchi na kundi la waasi.

Mapigano hayo yamezuka baada ya serikali kuanzisha oparesheni ya kuwasaka waasi wa ADF-Nalu, walioingia nchini humo kutoka Uganda.

Image caption Bendera ya Congo

Msemaji wa shirika hilo la Oxfam Elli Kemp aliambia BBC kuwa vijiji vingi vimeteketezwa katika mapigano hayo na kuwaacha watu bila makao.