Nilitekwa kwasababu za siasa: Amiri

Image caption Amiri arejea nyumbani

Mwanasayansi wa Nuclear kutoka Iran Shahram Amiri aliyetoweka mwaka mmoja uliopita akiwa hijja nchini Saudi Arabia na kutokea tena mjini Washington amewasili mjini Tehran.

Iran inadai kuwa mwanasayansi huyo alitekwa nyara na maafisa wa Marekani wa CIA, dai ambalo Marekani imekana.

Baada ya kulakiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Tehran, bwana Amiri alihutubia waandishi wa habari ambapo alikariri kuwa hajahusika kwa vyovyote na mpango wa nuclear wa Iran, na akasisitiza kuwa Marekani ilimteka nyara kwa sababu za kisiasa.

Image caption Amiri arejea nyumbani

Marekani imeshikilia msimamo wake kuwa Amiri alikwenda huko kwa hiari yake mwenyewe.