Tutawaangamiza hao AL Shabaab - Museveni

Image caption Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameapa kuwasaka na kuwamaliza wapiganaji wa Al-Shabaab. Museveni aliyasema hayo alipohutubia waandishi wa habari jana usiku katika mji wa Ntungamo mashariki mwa Uganda.

Aliongeza kuwa magaidi hao watasakwa nchini Uganda na pia nchini Somalia. Hii inafuatia arifa iliyotolewa mapema wiki hii na kundi hilo la Al-Shabaab kuwa walihusika na shambulio la bomu mjini Kampala lililowaua zaidi ya watu 70.

Image caption Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Museveni pia alitoa wito wa kuongezwa majeshi ya kuweka amani ya muungano wa Afrika AU, kufikia 20,000 kukabili makundi ya wapiganaji nchini Somalia ambayo amedai yanapata ufadhili kutoka Mashariki ya Kati.