Museveni: Tutawakamata hao Al-Shabaab

Image caption Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapa kuwasaka na kuwamaliza wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab. Museveni aliyasema hayo alipohutubia waandishi wa habari Jumatano usiku katika mji wa Ntungamo mashariki mwa Uganda.

Aliongeza kuwa magaidi hao watasakwa nchini Uganda na pia nchini Somalia. Hii inafuatia taarifa iliyotolewa mapema wiki hii na kundi hilo la Al-Shabaab kuwa walihusika na shambulio la bomu mjini Kampala lililowaua zaidi ya watu 70.

Museveni pia alitoa wito wa kuongezwa majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika, kufikia 20,000 kukabili makundi ya wapiganaji nchini Somalia ambayo amedai yanapata ufadhili kutoka Mashariki ya Kati.