Zimbabwe yapata rukhsa kuuza almasi

Image caption Machimbo ya alamsi Zimbabwe

Chombo kinachosimamia biashara ya "almasi haramu zinazotumika kugharamia vita" kimekubali kuwa Zimbabwe inaweza kuuza alamsi zake nje ya nchi kutoka machimbo mapya ya almasi mashariki mwa nchi hiyo.

Katika makubaliano hayo, Zimbabwe itaweza kuuza baadhi ya madini hayo.

Huenda uuzaji wake wa madini hayo nje ya nchi ukarejea baada ya masharti yake kupitiwa upya katika machimbo ya almasi huko Marange mwezi Septemba.

Kimberley Process ilizuia uuzaji wa almasi mwezi Novemba baada ya kuwepo madai ya kuwepo ukatili unaofanywa na majeshi ya usalama huko Marange.

Mazungumzo yamekuwa yakikwama katika wiki kadhaa juu ya makubaliano hayo na Urusi na kuibuka baada tu ya mtetezi wa haki za binadamu wa Zimbabwe alipoachiwa huru mapema wiki hii.

Farai Maguwu anashutumiwa kutoa taarifa za uwongo juu ya biashara hiyo ya almasi na kukamatwa baada ya kukutana na mwakilishi wa Kimberley Process Juni 3.

Kutiwa kwake kizuizini kulizuia jaribio la kufikia makubaliano ya uuzaji wa almasi nje ya Zimbabwe katika mkutano wa Kimberley Process huko Israel mwezi uliopita.

Kimberley Process iliundwa mwaka 2002 baada ya biashara ya almasi kushutumiwa kuchochea migogoro barani Afrika.