Chuki kwa wageni yafukuta Afrika Kusini

Image caption Jeshi lasaidia kuondoa Xenphobia

Jeshi la Afrika Kusini limeungana na polisi, kulinda doria mjini Johannesburg kutokana na mashambulio ya chuki dhidi ya raia wa kigeni yaliyosababisha watu saba kujeruhiwa vibaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni wahamiaji kutoka Zimbabwe na Msumbiji, pamoja na waafrika weusi wa Afrika Kusini waliojikuta katika mashambulio hayo jana usiku.

Katika barua kwa Rais Jacob Zuma, mkuu wa chama cha Democratic Alliance upande wa Western Cape, Hellen Zille alibaisha chimbuko la chuki dhidi ya wahamiaji weusi au Xenophobia. Hata hivyo hofu yake ilipuuzwa na mkuu wa polisi kama iliyokosa msingi.

Lakini sasa hivi imebainika wazi kuwa wageni kutoka Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na Nigeria, miongoni mwa nchi nyingine, wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa wakati wowote.

Tangu mashindano ya Kombe la Dunia kumalizika nchini Afrika Kusini, wageni wasiopungua 10 wameuawa na watu weusi wa Afrika Kusini katika sehemu ya Cape Town na hatari hiyo imeanza kuenea katika miji mingine.

Mkuu wa Polisi, Mbeki T'wele, ameahidi kuongeza idadi ya polisi wa kushika doria mitaani, kuimarisha usalama.