Uchaguzi wa Ubunge wakamilika Burundi

Raia wa Burundi
Image caption Raia wa Burundi

Uchaguzi wa ubunge nchini Burundi, umekamilika bila tukio lolote licha ya kuwepo ya wasi wasi nyingi kuhusu usalama.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Humo, idadi ndogo wa wapiga kura walijitokeza kushiriki kwenye zoezi hilo.

Msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo ameiambia shirika la habari la AFP kuwa matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutangazwa siku ya jumatatu.

Chama tawala cha CNDD-FDD kinatarajiwa kushinda idadi kubwa ya viti vya ubunge.

Vyama vingi vya upinzani vilisusia uchaguzi huo, vikidai uchaguzi wa hivi majuzi wa udiwani na urais uligubikwa na wizi wa kura.

Hali ya ulinzi umeimarishwa nchini Burundi, kufuatia vitisho vya mashambulio kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.

Burundi ni miongoni mwa nchi ambazo zimetuma wanajeshi wa kutunza amani nchini Somalia.