Rubani mmoja atekwa nyara na waasi Congo

Walinzi wa Usalama Congo
Image caption Walinzi wa Usalama Congo

Rubani mmoja raia wa India, ametekwa nyara na waasi, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo, waasi hao walishambulia uwanja mmoja mdogo wa ndege katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Generali Baigwa Dieudonne Amuli, ameiambia shirika la habari la Reuters, kuwa waasi wa Kihutu waliishambulia ndege moja kwa ushirikiano na waasi wengine katika eneo hilo na kumteka nyara rubani huyo, kabla ya kutoweka na kiasi cha pesa kisichojulikana.

Amulli amesema kikosi chake kwa sasa kinaendeleza msako dhidi ya waasi hao.

Waandishi wa habari wanasema uwanja huo wa ndege ulioko katika eneo la walikale hutumiwa kusafirisha madini ya chuma, kutoka mgodi ulioko katika eneo hilo.