Mkutano wa AU kuanza Kampala Uganda

Marais wa Afrika kwenye mkutano wa AU
Image caption Marais wa Afrika kwenye mkutano wa AU

Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Muungano wa Afrika, unaanza muda mfupi ujao mjini Kampala Uganda.

Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala kadhaa likewemo suala ya kodorora ya hali ya usalama na mzozo wa kisiasa nchini Somalia.

Mkutano huo wa AU, unajiri wiki mbili tu baada ya zaidi ya watu 76, kuuawa kwenye shambulio la bomu mjini Kampala. Uganda ni moja ya nchi ambayo imetuma wanajeshi wake kutunza amani nchini Somalia.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab wamedai kutekeleleza mashambulio hayo.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema viongozi wengi wanaohudhuria mkutano huo wanatarajiwa kuafiki wito wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni wa kuongeza idadi ya wanajeshi wa Kimataifa wa kutunza amani nchini Somalia.