Afghanistan: Mauaji ya NATO yafichuliwa

Majeshi ya NATO yameripotiwa kuwadhulumu raia wa Afghanistan
Image caption Majeshi ya NATO yameripotiwa kuwadhulumu raia wa Afghanistan

Mashirika makubwa matatu ya habari duniani yamechapisha kile yanachosema ni habari za kina zilizovuja za maelfu ya nyaraka za jeshi la Marekani katika vita vinavyoendelea nchini Afghanistan.

Magazeti haya, The Guardian, New York Times, na jarida la Ujerumani, Der Spiegel, yamesema, taarifa za kina za kijeshi zinaelezea kuuawa kwa maelfu ya raia wa Afghanistan na majeshi ya NATO, na wasiwasi wa NATO kwamba Pakistan na Iran zinawasaidia wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

Ikulu ya Rais nchini Marekani, White House imeshutumu kuchapishwa kwa taarifa hizo. Hata hivyo magazeti yanayayohusika yametaja hatua hiyo kama, 'kufichuka kwa habari kubwa zaidi katika historia ya kijasusi.'