Ajali ya ndege yaua watu 152 Pakistan

Ndege ya abiria imeanguka huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan na kuua watu wote 152 waliokuwa ndani yake.

Ndege hiyo, iliyokuwa katika safari kutoka Karachi kwenda Islamabad inaendeshwa na kampuni binafsi ya Airblue, ilianguka kwenye vilima vilivyoko kaskazini mwa jiji wakati ikijiandaa kutua.

Image caption Eneo la ajali hakifikiki kwa njia ya barabara, waokoaji walitumia mikono mitupu kufukua mabaki ya ndege.

Bofya hapa kuangalia picha zaidi

Hapakuwa na taarifa za awali kubaini chanzo cha ajali. Ingawa imeelezwa eneo hilo lilikuwa limetandwa na ukungu.

Televisheni za Pakistan zilionyesha picha za mabaki ya ndege yakiwaka moto, huku helikopta za uokoaji zikiranda juu.

Tathmini

Airblue ndiyo kampuni kubwa zaidi ya ndege binafsi, miongoni mwa mashirika yaliyoibuka nchini Pakistan katika miaka ya karibuni.

Kampuni hiyo na idara ya usimamizi wa safari za anga hawadhani ndege hiyo ilikutwa na matatizo ya kiufundi wakati ikiondoka Karachi.

Wanasema hapakuwa na dalili za hitilafu ya kiufundi katika mawasiliano kati ya rubani na mnara wa kuongozea ndege wa Karachi.

Hata hivyo, maafisa wa uwanja wa ndege waliieleza BBC kuwa ndege mbili zilizokuwa zitue kwenye mji huo mkuu zilikataliwa kabla ya ajali hiyo ya Airblue, katika ajali kubwa zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Pakistan.

Ingawa sekta ya safari za anga imekuwa kwa kasi, wakosoaji wanasema viwango vimekuwa chini na haviendani na ukuaji wa huduma.

Marubani hulalamika wanalazimishwa kuruka kwa saa za ziada, jambo linalosababisha uchovu, ingawa mashirika ya ndege yanakana madai hayo.

Image caption Ramani kuonyesha maeneo yanayohusiana na ajali ya ndege nchini Pakistan.

Jangwa kubwa

Imtiaz Elahi, mwenyekiti wa Capital Development Authority, mamlaka inashughulikia dharura, alisema ajali hiyo "inavunja moyo".

"Ni janga kubwa, na ninaweza kuthibitisha kwa uchungu kwamba hapakuwa na watu waliosalimika," alilieleza shirika la habari la Associated Press.

Ndege hiyo, inayosemekana kuwa ni muundo wa Airbus A321 ikiwa na abiria 146 na wafanyakazi sita ndani yake, inaaminika kuwa iliondoka Karachi saa mbili kasorobo asubuhi majira ya huko.

Hakuna walionusurika

Awali, Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, ilisema watu wasiopungua watano walikuwa wamenusurika kifo na kupelekwa hospitalini, lakini maafisa wa maeneo hayo baadaye walisema taarifa hizo hazikuwa sahihi.

Televisheni za maeneo hayo zilionyesha vipande vya mabati na chuma vikining'inia kutoka juu ya miti na kutapakaa ardhini.Kifaa cha kutunza kumbukumbu za safari kimekwishapatikana.

Maafisa wanasema waokoaji waliokuwa wakitafuta watu walionusurika, walikuwa wakitumia mikono mitupu kufukua mabaki hayo. Eneo la ajali lililoko kwenye mlima mkali, halifikiki kwa barabara.

Bofya hapa kuangalia picha za ajali hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii