Kocha wa Argentina Maradona atimuliwa

Maradona ametimuliwa kama kocha wa Argentina
Image caption Maradona ametimuliwa kama kocha wa Argentina

Shirikisho la soka la Argentina limemtimua mchezaji wao mashuhuri wa zamani Diego Maradona kama kocha wa timu ya taifa.

Inaripotiwa kuwa Diego Maradona au alivyotambuliwa kufuatia kombe la dunia la mwaka 1986 ''mkono wa mungu'', alitimuliwa baada ya kukataa masharti aliyopewa ili aongezewa mkataba.

Mojawapo ya masharti hayo, ni kuwashirikisha wasaidizi wenye utalaam wa soka , jambo alilolikataa.

Mambo yalianza kumwendea mrama Maradona pale timu yake ya Argentina ambayo ilikuwa imepigiwa upatu kunyakuwa ubingwa wa kombe la Dunia huko Afrika Kusini , ilipobanduliwa na Ujerumani kwa mabao 4 -0 katika hatua ya robo fainali.