Mafuriko yawaua zaidi ya watu laki moja Pakistan

Zaidi ya watu laki moja wamefariki nchini Pakistan kufuatia mafuriko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Kulingana na maafisa wakuu wa serikali, maelfu ya wengine wamekwama katika maeneo yaliyofurika.

Aidha Jeshi la nchi limelazimika kusaidia katika juhudi za uokozi huku Marekani ikiahidi kutoa msaada wa dharura wenye thamani ya dola milioni kumi.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu, Mike O'Brien alifahamisha BBC kuwa athari za mafuriko hayo huenda zikadumu kwa muda mrefu.

Halikadhalika, mimea na vyakula shambani viimeathrika huku hofu ikitanda ya muda wa kuweza kupanda tena chakula ukiyoyoma.