Waziri Swazi ajiuzulu kwa ugoni wa kifalme

Mfalme Mswati III
Image caption Mfalme Mswati III

Waziri wa sheria wa Swaziland amejiuzulu kufuatia madai kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja miongoni mwa wake 13 wa Mfalme Mswati III.

Waziri mkuu alisema Ndumiso Mamba amejiuzulu nafasi zake zote mbili za uwaziri na useneta

Alisema ni kwasababu ya " madai yanayosambaa nchini humo."

Waandishi wanasema madai ya uhusiano wa Bw Mamba na malkia Nothando Dube yaliripotiwa awali katika vyombo vya habari vya nchi jirani ya Afrika Kusini.

Mke wa 12 wa mfalme huyo ameripotiwa kukana madai hayo na Bw Mamba hajasema lolote hadi sasa.

Lakini waziri mkuu Sibusiso Dlamini alisema Bw Mamba alikubali kuachia madaraka ili madai hayo yachunguzwe.

Baadhi ya Waswazi humkosoa sana mfalme Mswati- utawala wake wenye kuwa na matumizi makubwa kupita kiasi na wake wengi haulingani kabisa na umaskini uliopo nchini mwake.