Maharamia waikimbia meli waliyoiteka

Maharamia
Image caption Maharamia wa Kisomali

Maharamia wameikimbia meli waliyoiteka, siku moja baada ya kufanya hivyo kwenye Ghuba ya Uajemi. Habari hizi ni kwa mujibu wa jeshi la Umoja wa Ulaya linalofanya doria katika eneo la pwani ya Somalia.

Mabaharia wawili kati ya 22 wanaofanya kazi katika meli hiyo wamejeruhiwa wakati wa shughli ya utekaji nyara. Mabaharia hao ni raia wa Syria na Misri.

Afia wa Umoja wa Ulaya amesema wanawapa mabaharia hao wawili matibabu.

Maharamia hao, ambao walikitekeleza chombo walichokuja nacho, waliondoka na boti wa dharura ya meli hiyo.