Pakistan yakatishwa tamaa na jamii ya kimataifa

Mafuriko Pakistan
Image caption Mafuriko Pakistan

Maafisa waandamizi katika serikali ya Pakistan wamekosoa kile walichosema kujivuta kwa jamii ya kimataifa katika kutoa msaada, kufuatia janga la mafuriko lililoikumba nchi hiyo, ambalo ndiyo baya zaidi kuwahi kutokea katika historia.

Balozi wa kudumu wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Zamir Akram, aliambia BBC kuwa wakati ukubwa wa uharibifu huo ulitambulika, hadi sasa hakuna msaada wa kutosha uliowafikia waathiriwa.

Alisema kuwa watu millioni kumi na nne waliathiriwa, wakati kukiwa na hofu ya ya mafuriko mapya katika majimbo ya Punjab na Sind.

Mashirika ya misaada yametoa onyo jipya kuhusu matatizo ya kiafya yaliyosababishwa na ukosefu wa maji safi ya kunywa.