Obama aunga mkono Waislamu Marekani

Obama na Waislamu
Image caption Obama na Waislamu

Rais Obama ameunga mkono mipango yenye utata ya Waislamu mjini New York kutaka kujenga kituo cha kitamaduni na msikiti karibu na eneo la mashambulizi ya Sept 11,mwaka wa 2001,ambapo watu zaidi ya elfu tatu waliuwawa.

Wanaopinga mpango huo wamesema hatua hiyo ni utovu wa heshima na kutojali kwa kumbukumbu za waliopoteza maisha yao.

Lakini Rais Obama akizungumza kwenye hafla ya futari ya Waislam kwenye ikulu ya Marekani, White House, alisema anaamini kuwa Waislamu wana haki ya kufanya ibada kulingana na dini yao sawa na mtu mwingine yeyote, na hiyo ni pamoja na haki ya kujenga mahali pa ibada.

Alisema malengo ya Al-Qaida ni kinyume na Uislamu halisi, na wale wanaounga mkono kikundi hicho ni magaidi ambao waliwauwa watu wasiokuwa na hatia.