Mgomo watatiza shughuli SA

Wafanya kazi wa umma wanadai nyongeza
Image caption Wafanya kazi wa umma wanadai nyongeza

Mgomo wa wafanyikazi wa umma nchini Afrika Kusini umeingia siku yake ya pili, huku wafanyikazi zaidi wakitarajiwa kujiunga na mgomo huo, ambao umekatiza hudumu za umma kote nchini humo.

Imetangazwa kwamba wanachama laki moja wa muungano wa wafanya kazi wa umma ambao hawakugoma jana watajumuika na wenzao hii leo kudai nyongeza ya mishahara.

Vyama vya wafanya kazi nchini humo vimetishia kufunga mojawapo wa barabara kuu na yenye shughuli nyingi sana katika mji mkuu wa Johannesburg kuishinikiza serikali kuwaongezea mishahara.

Zaidi ya wafanyikazi millioni moja wakijumuisha madaktari, wauguzi, maafisa wa polisi na walimu wamegoma wakitaka nyongeza ya mishahara ya asilimia nane nukta sita badala ya asilimia saba iliyopendekezwa na serikali.