Pweza Paul aiunga mkono Uingereza

Image caption Pweza, Paul

Yule pweza aliyetabiri kwa uhakika matokeo ya mechi zote ambazo timu ya Ujerumani ilishiriki katika mashindano ya fainali za Kombe la Dunia huko Afrika kusini na pia kuwa Uhispania itashinda mechi ya fainali, ameibuka tena.

Ameajiriwa kuwa balozi wa Uingereza kusaidia juhudi za kufanikisha ombi la nchi hiyo kuandaa fainali za mwaka 2018.

Pweza huyo maarufu kama Paul, alistaafu kufanya utabiri wa mchezo wa mpira wa miguu, lakini ameonekana katika video mpya kwenye kampeni ya England kuandaa fainali za mwaka 2018.

Tangu hapo kiumbe huyo wa baharini ana asili hapa England ya kusini ingawa baadaye aliununuliwqa na kituo cha Uhai wa Baharini kilichoko huko Ujerumani.

Katika video ya kutangaza juhudi za England, mnyama huyo aliyetajwa kama wa ajabu mwenye miguu minane, anaonekana akitoka kwenye tengi lake na kushika tengi lenye rangi na nembo ya bendera ya England ikiwa na maandishi ya England 2018.