Wananchi wa Australia wapiga kura

Gillard na Abbott
Image caption Gillard na Abbott

Upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Australia unaendelea.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa matokeo yatakuwa karibu mno kuwahi kupatikana katika miaka ya hivi karibuni, kukiwa na uwezekano wa kuundwa kwa bunge ambalo hakuna chama chenye uwingi wa viti.

Kampeni zimetawaliwa na sifa za , Julia Gillard, wa chama tawala cha Labor, ambaye ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Australia.

Bi Gillard alimwondoa mtangulizi wake, Kevin Rudd, miezi michache iliyopita.

Chama chake kinatarajia kushinda mhula wa pili kutokana na jinsi kinavyoshughulikia uchumi.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha muhafidhina (conservative),Tony Abbot, ametumia vizuri mgawanyiko ulio ndani wa chama cha Labor, kufuatia mabadiliko ya ghafla ya uongozi.