Maaskofu wa kianglikana barani Afrika wakutana Uganda

Image caption Kiongozi wa kanisa la Anglikana Rowan Williams

Zaidi ya Maaskofu 20 kutoka majimbo zaidi ya 400 ya kianglikana barani Afrika leo wanaanza mkutano wao wa wiki moja mjini Kampala Uganda.

Mkutano huo unafanyika siku kadhaa baada ya askofu mkuu wa Uganda, Henry Luke Orombi, kusema kuwa kanisa la kianglikana limekuwa familia isiyo na mshikamano na ambalo limepoteza hadhi yake.

Maaskofu hao wanatarajiwa kujadili masuala mbali mbali ya kanisa hilo, yakiwemo mizozo ndani ya kanisa, umaskini, utawala na changamoto zingine zinazolikabili.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mgawanyiko kati ya kanisa la kianglikana barani Afrika na baadhi ya makanisa ya Marekani na ulaya kuhusu suala la kuwatawaza wapenzi wa jinsia moja kuwa maaskofu.