Pakistan kuomba msaada kwa IMF

Maji ya mafuriko

Wakati Pakistan ikikabiliwa na moja ya maafa makubwa katika karne hii, maafisa wa nchi hiyo wameanza mazungumzo mjini Washington na shirika la fedha duniani IMF.

Kabla ya kutokea kwa mafuriko hayo , mazungumzo baina ya pande hizo mbili yalijikita juu namna ya kuipatia Pakistan mkopo wa muda mfupi kwa awamu.

Lakini waandishi wa habari wanasema kwa sasa Pakistan huenda ikaomba mkopo wa dharura.

Tume ya Pakistan ya kukabiliana na mafuriko inasema mto Indus uliopo nj kidogo ya mji wa hyderabad katika jimbo la Sindh umejaa maji kwa kiwango cha hali ya juu kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi y miaka hamsini, na unatarajiwa kufurika maji zaidi hii leo.

Umoja wa mataifa unasema licha ya kwambaumweza kukusanya asilimia sabini ya fedha uliohitajika kwa msaada , watu wengi bado hawajabata msaada wowote.

Serikali ya pakistan inakadiria kuwa ukarabati wa nchi hiyo utagarimu takriban dola bilioni kumi na tano.