Tiger Woods na mkewe watalikiana

Tiger na Elin kabla ya kutengana

Bingwa wa mchezo wa Golf duniani Tiger Woods ametalikiana na mkewe Elin Nordegren.

Hayo yalibainika katika taarifa ilotumwa kwenye mtandao wa mchezaji golf huyo namba moja duniani.

Kwa pamoja walisema "Tunasikitika kuwa ndoa yetu imefikia tamati na tunatakiana kila la heri katika mustakabala wetu," wawili hao walisema.

Hata hivyo wanasema watasaidiana majukumu ya kulea watoto wao wawili.Suala la kugawana pesa halijawekwa wazi lakini taarifa katika vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa bi.

Nordegren huenda akaondoka na kitita cha dola milioni 100.Naam ni ya Woods na mtalaka wake.

Woods amekuwa na matatizo kwenye ndoa yake baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.