Ajali ya ndege yaua 19 Kongo

Image caption Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Maafisa wamesema, ndege moja imepata ajali magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuua raia 19.

Kanali Joli Limengo, mkuu wa polisi katika jimbo la Bandundu, ameliambia shirika la habari la AP kwamba watu wawili wamenusurika kwenye ajali hiyo.

Msemaji mmoja wa Umoja wa Mataifa alisema ndege hiyo ilianguka kwenye nyumba karibu na mji wa Bandundu.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ina ukubwa wa magharibi mwa Ulaya ina barabara chache baada ya miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ina rekodi mbaya ya usalama wa angani duniani.

Msemaji wa umoja huo Madnodje Mounoubai amesema abiria waliopo kwenye ndege hiyo na wengine waliokuwa barabarani wamefariki dunia.

Polisi wamesema miili ya watu 19 imetolewa kwenye eneo la ajali hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikisimamiwa na shirika la nchini humo liitwalo Filair na ilipitia Bandundu ikielekea kwenye mji mkuu wa Kinshasa.