Gaddafi ataka Ulaya iilipe Libya k

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, amesema Muungano wa Ulaya (EU)unapaswa kuilipa Libya takriban dola bilioni 6.3 kila mwaka ili kukomesha wahamiaji haramu Waafrika na kuepuka "Ulaya nyeusi" .

Akiongea wakati wa ziara yake nchini Italia, Kanali Gaddafi alisema Ulaya "inaweza kugeuka Afrika" kwa kuwa kuna "mamilioni ya Waafrika wanaotaka kuja"

Italia imeshutumiwa kwa kuwakabidhi Libya wahamiaji inaowakamata katika bahari yake kabla kwanza ya kuwachuja.

Matokeo yake ni kwamba wakimbizi wachache zaidi huwasili Italia kutokea Libya. Takwimu za Muungano wa Ulaya zaonyesha kuwa mnamo mwaka 2009 idadi ya watu waliokamatwa wakijaribu kuingia Italia kwa njia ya haramu ilipungua kufikia 7,300, kutoka 32,052 mnamo mwaka 2008.

Kanali Gaddafi ameimarisha uhusiano wa karibu sana na Italia tangu kutia saiani mkataba wa amani miaka miwili iliyopita uliokusudiwa kuondoa chuki za kihistoria kati ya Libya na Italia iliyokua mtawala wake wa kikoloni. .

"Kesho Ulaya huenda isiwe tena ya wazungu kwa kuwa kuna mamilioni wanaotaka kuingia. Hatujui kile kitakachotokea; hatujui wakristo wazungu watafanya nini watakapokabiliwa na mmiminiko huu wa Waafrika wajinga na wenye njaa, " alisema Kanali Col Gaddafi, aliyenakiliwa na shirika la habari la AFP.

Alikuwa akiongea katika sherehe za mjini Roma zilizohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi.

Ziara ya Kanali Gaddafi iligubikwa na hotuba yake nyingine iliyozusha ubishi mkubwa kwa vikundi viwili vya wanawake nchini Italia, ambao walilipwa euro 70 na 80 kila mmoja, akiwambia kwamba dini ya kiislamu inapaswa kuwa dini ya bara la Ulaya na kuwapa nakala za Quraan baada ya kuwahubiria kwa muda wa saa nzima kuhusu uhuru walio nao wanawake wa Libya.