Rwanda yahimizwa kubadili sheria zake

Miili ya watu waliouawa nchini Rwanda
Image caption Miili ya watu waliouawa nchini Rwanda

Shirika la kutetea haki za kibinadam la Amnestry International, limetoa wito kwa serikali ya Rwanda kuchunguza upya sheria zake kuhusu mauaji ya kimbari au genocide, ambazo zinatumiwa kuwakandamizi wapinzani wa serikali.

Shirika hilo la linasema, maneno yanayotumiwa kwenye sheria hizo zinazopiga marufuku, utumizi wa fikra zinazowakumbusha watu mauaji ya kimbari na sera za ubaguzi, yameipa utawala wa nchi hiyo fursa ya kuyatumia vibaya, kuwakandamizi wanasiasa wa upinzani na kuzuia uhuru wa kuongea.

Sheria hizo zilibuniwa baada ya mauaji ya kimbari ya 1994. Serikali ya Rwanda imesema sheria hizo ni muhimu, ili kuhakikisha uthabiti. Hata hivyo Utawala wa nchi hiyo umeshutumiwa kwa kutumia sheria hizo kuwakandamiza wapinzani wake, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

Rais Paul Kagame alishinda uchaguzi huo kwa idadi kubwa ya Kura.