Mgomo wa wafanyakazi unaendelea-SA

Mazungumzo kati ya serikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini yanaendelea ili kujaribu kumaliza mgomo wa wafanyakazi wa uma kuhusu nyongeza ya mishahara.

Mazungumzo hayo yalianza jana kufuatia agizo la Rais Jacob Zuma kwa mawaziri wake, kumaliza mzozo huo ambao umesababisha shule kufungwa, kutatizika kwa huduma za afya na kuongezeka kwa viwango vya ufisadi nchini humo.

Image caption Wafanyakazi wanaogoma nchini Afrika Kusini

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema serikali ya nchi hiyo imekubali kuwapa wafanyakazi hao nyongeza zaidi ya mishahara.

Vyama vya wafanyakazi nchini humo vinadai nyongeza ya asilimia 8.6 na kuongezwa kwa marupurupu ya nyumba.