Idadi ya waliobakwa DRC yaongezeka

Wanajeshi wa waasi nchini Congo
Image caption Wanajeshi wa waasi nchini Congo

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya waathiriwa wa ubakaji wa halaiki katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeongezeka kwa zaidi ya visa mia moja.

Wanajeshi wa Umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUC, wamesema wamepokea ripoti zaidi na kufikisha idadi ya watu wanaodai kubakwa kuwa 240.

Wapiganaji wa waasi nchini Rwanda na Congo wanatuhumiwa kutekeleza mashambulio hayo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini wiki 4 zilizopita.

Umoja wa Mataifa umeshutumiwa kwa kutofanya juhudi zaidi ili kuzuia tukio hilo ambalo lilitokea takriani kilomita 30 kutoka kwa kambi ya wanajeshi wake.

Lakini Umoja huo unasema wanajeshi wake walipokea habari siku kumi baada ya tukio hilo kutokea.