Hamas kuendelea kuwashambulia Waisraeli

Hamas
Image caption Viongozi wa Hamas

Kundi la wapiganaji la Palestina lenye silaha, Hamas, limeonya kwamba litaendelea kuwashambulia Waisraeli popote pale walipo katika Ufuko wa Magharibi.

Wakuu wa kundi hilo la Hamas wameelezea kwamba walihusika katika kuwapiga risasi na kuwajeruhi wanajeshi wawili wa Israel, huku viongozi wa Palestina na Israel wakikutana mjini Washington katika mazungumzo ya ana kwa ana, hii ikiwa ni mara ya kwanza wao kukutana hivyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kundi la Hamas, ambalo halijaalikwa katika mashauri hayo ya amani, limesema kwamba kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, hana madaraka ya kuendelea na mashauri kwa niaba ya Wapalestina.

Siku ya Jumanne kundi la Hamas liliwaua masetla wanne wa Israel katika Ufuko wa Magharibi.