Rais Banda aondolewe madarakani-Bwalya

Rais wa Zambia
Image caption Rais wa Zambia

Nchini Zambia kasisi mmoja wa kanisa la Katoliki na mwanaharakati wa kisiasa Padre Frank Bwalya, amesema wabunge wa nchi hiyo wanapaswa kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani na rais Rupiah Banda.

Bwalya ameyasema hayo baada ya mahakama moja nchini humo kutupilia mbali kesi ambayo ingelimlazimisha rais wa zamani wa nchi hiyo, Fredrick Chiluba, kulipa mamilioni ya dola ambazo anatuhumiwa kuiba wakati alipokuwa madarakani.

Utawala wa rais Banda umekataa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Kasisi Bwalya alianzisha kampeini ya kadi nyekundu dhidi ya serikali ya nchi hiyo mapema mwaka huu ili kuonyesha kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wake.