Uchaguzi kufanyika Octoba-Ivory Coast

Ramani ya Ivory Coast
Image caption Ramani ya Ivory Coast

Uchaguzi wa Urais uliokuwa umechelewesha mara kadhaa nchini Ivory Coast, sasa huenda ukaandaliwa baada ya tume ya uchaguzi nchini humo, kwa mara ya kwanza kuidhinisha daftari rasmi ya wapiga kura.

Kadi za kupigia kura zinatarajiwa kuchapishwa mwezi huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo tarehe 31 mwezi ujao.

Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika miaka mitano iliyopita wakati muda wa kuhudumu wa rais wa nchi hiyo ulipomalizika lakini umehairishwa mara kadhaa.

Mzozo kati ya rais Laurent Gbagbo na vyama vya upinzani kuhus daftari la wapiga kura, umechangia pakubwa kuhairishwa kwa uchaguzi huo.