Nigeria yatabiri uchumi wake kukua mwaka 2012

Sarafu ya Nigeria
Image caption Sarafu ya Nigeria

Waziri wa fedha wa Nigeria, Olusegun Aganga, ametoa makadirio yenye kutia moyo ya hali ya uchumi , akisema anatarajia ukuaji wa kasi wa uchumi wa nchi yake ifikapo mapema mwaka wa 2012.

Akizungumza kwenye mkutano wa uchumi uliofanyika mjini London, Bw Aganga alisema wakati uchumi wa Ulaya na Marekani ukikua kwa mwendo wa pole, kuna wawekezaji wakubwa duniani wanaokuja Nigeria kila wiki.

Mhariri wa BBC anasema ikiwa utabiri wa waziri utakuwa kweli basi hali hiyo itabadili hali ya maisha ya ya raia millioni 160 wa nchi hiyo.

Mhariri huyo ameongeza kuwa Nigeria iliwahi kuwa mfano wa visa vya kupindua serikali na ufisadi.

Lakini sasa inajiweka katika nafasi ya kuwa kivutio kwa wawekezaji, kubinafsisha secta ya umeme na kutenga fungu kubw ala mipango ya kuendeleza miundo mbinu yake.