Mwanaharakati adai kutekwa, kuteswa DRCongo

Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Image caption Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Mwanaharakati wa haki za kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekishtumu kikundi cha zamani cha waasi, CNDP, kwa kumteka nyara na kumtendea vibaya.

Mwanaharakati huyo, Sylvestre Bwira, aliambia BBC kuwa alitekwa nyara baada ya kumwandikia barua Rais Joseph Kabila, kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu uliofanywa na kundi la Watutsi mashariki mwa Congo.

Alisema wakati akishikiliwa mateka kwa wiki moja aliwekwa sehemu iliyo chini ya ardhi na kukalishwa juu ya mifupa ya binadamu.

Serikali ya jimbo la Kivu ya Kaskazini ilisema inachunguza madai hayo ya utekaji nyara na iliimarisha ulinzi wa wanaharakati kama vile Bw Bwira.