Kashfa ya kupanga matokeo ya cricket Uingereza

Wachezaji wa cricketi wa Pakistan
Image caption Wachezaji wa cricketi wa Pakistan

Gazeti moja la Uingereza limetoa madai mapya kuhusu kashfa ya kupanga matokeo ya mechi inayomhusisha mchezaji cricketi wa Pakistan.

Gazet hilo, The News of the World linadai Baraza la Kimataifa la Cricket -lCC-linamchunguza mchezaji huyo, ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kisheria.

Baraza la ICC limesema haliwezi kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi unaondelea.

Hatua ya kupanga matokeo ya mechi ni nzito kuliko madai yaliyotolewa na gazeti hilo wiki iliyopita.

Gazeti hilo lilifichua kashfa ya kamari ambayo ilisababisha wachezaji watatu wa timu ya Pakistan kusimamishwa na wanafanyiwa uchunguzi na Baraza la Kimataifa la Cricketi pamoja na polisi.