Mlipuko waangamiza watoto Pakistan

Uharibifu uliofanywa na bomu
Image caption Kati ya waliokufa ni watoto na maafisa wa polisi

Watoto wanne waliokuwa wakielekea shule ni kati ya watu 19 waliokufa kutokana na mlipuko wa bomu katika eneo la kaskazini-magharibi nchini Pakistan.

Mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga, akiendesha gari aina ya pickup, alikishambulia kituo cha polisi katika mji wa Lakki Marwat, katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa.

Vitabu na mikoba ya shule ilitawanyika katika eneo hilo.

Taarifa zinaelezea kwamba kati ya waliokufa ni maafisa 11 wa polisi.

Zaidi ya watu 100 walikufa katika mashambulio dhidi ya Washia wiki iliyopita.

Wataleban waliopo nchini Pakistan walisema walihusika na mashambulio hayo.

Baada ya hali ya utulivu kufuatia mafuriko ya hivi karibuni nchini Pakistan, inaelekea wapiganaji nchini humo sasa wameanza tena mashambulio yao.