Wafanyakazi Afrika kusini waakhirisha mgomo

Image caption Wafanyakazi wa umma Afrika kusini

Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Afrika kusini, wanatarajiwa kuanza kurejea kazini leo siku moja baada ya kuakhirisha mgomo wao wakidai malipo yao ya mwezi mmoja.

Wakuu wa vyama vya wafanyakazi, walisema kuwa walikataa kukubali pendekezo la serikali kuongeza mishahara yao ingawa walikubali kusitisha mgomo wao kwa wiki tatu kuruhusu viongozi wao kutafakari pendekezo la serikali.

Wachunguzi wanasema kuwa mgomo uliosababisha kufungwa kwa hospitali na shule umeathiri ushirikiano wa kisiasa kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi. Wakati huohuo, serikali inadaiwa imepata hasara ya dola milioni miamoja arobaini kutokana na mgomo huo.