Ban ki Moon kukutana na Kagame

Image caption Rwanda

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, anatarajiwa kukutana na rais wa Rwanda, Paul Kagame, mjini Kigali baadaye leo.

Lengo kuu likiwa kupunguza wasiwasi uliopo kuhusu ripoti ya umoja huo iliyofichuliwa , ikiwanyoshea kidole wanajeshi wa Rwanda kwa madai ya kufanya mauaji ya kimbare.

Kwa upande wake, Rwanda imetishia kuondoa wanajeshi wake walio miongoni mwa kikosi cha wanjeshi wa amani wa umoja Mataifa nchini Sudan kwa sababu ya madai ya ripoti hiyo kuwa wanajeshi wa Rwanda waliwaua maelfu ya wahutu waliokimbilia nchini Congo miaka ya tisini.

Msemaji wa bwana Ban, Yves Sorokobi, aliambia BBC kuwa ni jambo la kusikitisha ripoti hiyo ilifichuliwa.

Kulingana naye , bwana Ban alienda Rwanda kusikiza namna serikali ilivyodurusu rekodi ya haki, za kibinadamu mashariki mwa Congo.

Kuchapishwa kwa ripoti hiyo sasa kumeakhirishwa hadi mwezi Oktoba.