Migodi yafungwa mashariki mwa Congo

Uchimbaji madini DR Congo
Image caption Uchimbaji madini DR Congo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, ameamuru kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji migodi katika majimbo matatu mashariki mwa nchi.

Maafisa wa serikali ya Congo walisema hatua hiyo inalenga kukwamisha shughuli za waasi wenye silaha katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini, Kivu ya Kusini na Maniema.

Makundi ya waasi yanaendesha kampeni za kijeshi dhidi ya serikali katika eneo hilo.

Makundi ya haki za binadamu yameshtumu pande zote katika mgogoro huo, serikali na waasi kwa kukiuka haki za binadamu, pamoja na kujinufaisha na mapato ya madini ili kufadhili harakati zao.