Viongozi wakutana juu ya LRA ya Uganda

Waasi wa LRA
Image caption Waasi wa LRA

Viongozi wa kisiasa na wa kidini kutoka mataifa manne ya KiAfrika yaliyoathiriwa na uasi wamesema mashambulizi yanayoendelea ya kundi la Lord's Resistance Army la Uganda yanaweza kuathiri vibaya kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika juu ya uhuru wa eneo la Sudan Kusini.

Wawakilishi hao kutoka Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati walisema Umoja wa Mataifa na serikali husika zinapaswa kufanya juhudi zaidi za kuwalinda raia.

Walikuwa wakizungumza siku ya mwisho ya mkutano wa siku tatu kujadili suala la kundi la Lord's Resistance Army uliofanyika mjini Yambio Sudan Kusini.