Kura ya maoni kufanyika Uturuki

Kura ya maoni ya katiba ya Uturuki
Image caption Kura ya maoni ya katiba ya Uturuki

Kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba inafanyika nchini Uturuki, ambapo serikali inadai marekebisho hayo yanahitajika kuimarisha demokrasia na kusukuma mbele azma ya serikali ya kutaka kuwa mwanachama wa Muungano wa Ulaya.

Katiba ya sasa iliandikwa wakati Uturuki ikiwa chini ya utawala wa kijeshi mapema miaka ya elfu moja mia tisa na thamanini.

vyama vya upinzani vinakishtumu chama tawala cha Justice and Development party -- ambacho kina misingi ya sera za kisiasa zinazoegemea Uislam--kwa kushinikiza marekebisho hayo ili kiweze kizatiti udhibiti wake wa mahakama nchini humo.

Mwaka wa 2008, chama hicho tawala kiliponea chupu chupu kupigwa marufuku na Mahakama ya Katiba kwa kudaiwa kutatiza mfumo wa kisiasa usio na misingo ya kidini unaotumika Uturuki.

Kura hiyo ya maoni inatarajiwa kutoa matokeo yanayokaribiana.