Ghasia zaidi Kashmir

Kashmir
Image caption Zaidi ya watu 15 wamekufa katika ghasia za Kashmir

Maafisa wa polisi wamewapiga risasi na kuwaua zaidi ya raia 15, katika ghasia mbaya zaidi kutokea katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wakati wa maandamano katika eneo linalosimamiwa kiutawala na India, Kashmir.

Afisa mmoja wa polisi pia alifariki baada ya kugongwa na lori.

Mwandishi wa BBC mjini Srinagar, Altaf Hussain, alisema maandamano hayo yalizuka kutokana na gadhabu dhidi ya taarifa kwamba Kuran zingeliteketezwa nchini Marekani.

Watu kadhaa katika jimbo la Kashmir sasa wamekuta tangu mwezi Juni, katika maandamano ya kuipinga India, baada ya kijana mmoja kupigwa risasi.