Rwanda haitishwi na mahakama za Ufaransa

Image caption Rwanda

Serikali ya Rwanda imesema haitatishwa na uamuzi wa mahakama ya rufaa nchini Ufaransa wa kukataa kuikabidhi daktari mmoja anayesakwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994. Mahakama hiyo imesema mshukiwa huyo hawezi kupata haki wakati wa kesi dhidi yake.

Dk Eugene Rwamucho alikamatwa Ufaransa mwezi Mei mwaka huu baada ya kutolewa kibali cha kimataifa. Amekanusha kuhusika na mauaji hayo.

Utawala wa Rwanda hata hivyo unasema utaendelea kushinikiza jamaa huyo kukabidhiwa kwake.